Guerrero Ahukumiwa Kutocheza

Paolo Guerrero kwa sasa hataweza kuichezea timu yake mpya ya International kutoka Brazili kutokana na hukumu aliyopewa inayoimzuia kucheza soka kutokana na matumizi ya dawa za kulevya. Awali mkali huyu alifeli kipimo cha matumizi ya dawa za kulevya hivyo angeshindwa kutinga katika fainali za kombe la dunia kule Urusi. Lakini kwa mujibu wa FIFA mahakama moja ya nchini Uswiswi ilitoa maamuzi ya kisheria yaliyomruhusu Paolo Guerrero  kucheza katika fainali za kombe la dunia kule Urusi.

Mahakama kuu ya nchini uswiswi imetoa zuio la Paolo Guerrero  kucheza hivyo kuathiri mkali huyu kuichezea timu yake mpya. Paolo Guerrero  ambaye ana umri wa miaka 34 sasa mwanzo alipewa adhabu na FIFA ya kipindi cha mwaka mmoja na baadae kupunguziwa kuwa miezi 6.  Lakini mahakama ya michezo nchini Uswiswi (CAS) ilitoa hukumu tena ya miezi 14 kutoka miezi 6 iliyotolewa na fifa, mpaka sasa Paolo Guerrero  anasubiri maamuzi ya mwisho katika rufaa aliyowasilisha mahakamani kupinga adhabu ya miezi 14 aliyopewa na CAS.

 

 

Makala iliyopita

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.