Cristiano Ronaldo kama atafanikiwa kucheza michuano ya EURO, 2020 ambapo mchezo wao Portugal vs Hungary utapigwa kesho, basi anaweza kuvunja rekodi zifuatazo:
1️⃣- MCHEZAJI ALIYECHEZA MASHINDANO MENGI ZAIDI YA EURO :
Ronaldo ni moja kati ya wachezaji 17 waliowahi kushiriki michuano ya EURO kwa vipindi vinne tofauti (2004, 2008, 2012, na 2016). Lakini Ronaldo kesho akifanikiwa kucheza atakuwa anaingia katika Vitabu vya Rekodi kwa kucheza michuano hii x 5 [2004, 2008, 2012, 2016 & 2020🔜]
2️⃣- MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE WA UEFA EURO :
Cristiano : Goli 9
Michel Platini : Goli 9
Mpaka sasa Ronaldo amefunga Mabao 9 katika michuano hii huku nyuma yake kwa wachezaji wanaoendelea kucheza Soka ni Antoine Griezmann (6), hivo Ronaldo ana nafasi kubwa ya kuweka rekodi mpya kwenye mashindano haya ya kuwa Mfungaji bora wa muda wote wa michuano hii.
3️⃣- MCHEZAJI ALIYECHEZA MECHI NYINGI ZA EURO [+Mechi za kufuzu]
Gianluigi Buffon (Italy–Mechi 58 )
Cristiano (Portugal–Mechi 56)
Mario Frick (Liechtenstein–Mechi 51)
Cristiano anahitaji michezo mitatu kuweka rekodi mpya ya kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi UEFA EURO.
4️⃣- NAHODHA ALIYESHINDA TAJI LA EURO KATIKA FAINALI MBILI MFULULIZO:
Kama URENO watafanikiwa kutetea Taji la UEFA EURO 2020, Ronaldo Ataingia kwenye vitabu vya kumbukumbu pamoja na Iker Casillas kuwa Manahodha wawili pekee waliofanikiwa kuziongoza timu zao kutwaa Taja hili kwa mara mbili mfululizo, ambapo Casillas aliiongoza Hispania kutwaa taji hilo 2008 & 2012.
5️⃣- MFUNGAJI MWENYE UMRI MKUBWA KATIKA MICHUANO YA EURO :
Kama Cr7 atafanikiwa kufunga goli kwenye michuano hii, ataweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga Goli kwenye michuano ya EURO, rekodi ambayo kwa sasa inashikiliwa na mchezaji wa zamani wa West Germany Bernd Holzenbein aliyefunga goli katika Mashindano ya EURO 1976 akiwa na umri wa miaka 30 na siku 103.
Haya Yanaweza kuwa mashindano Ya mwisho makubwa kwa Cristiano Ronaldo aliye na miaka 36 kwa sasa, kuiwakilisha Timu ya Taifa ya URENO.
Hizi ni takwimu na rekodi bomba sana ambazo zimeletwa na moja ya wachambuzi wa soka nchini Tanzania.
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑



Hope mwaikuka
Jamaaa yuko vzur
Angelina
Namkubali
magdalena
Safii