Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Tetesi zinasema, Sancho atapatiwa jezi namba 7 katika klabu ya Manchester United ambayo kwa sasa inavaliwa na mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34.

United pia ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich Leon Goretzka, 26, ambaye kandarasi yake na klabu hiyo ya Bundesliga inakamilika 2022.

Tetesi zinasema, Manchester United na Liverpool huenda wakamkosa winga wa Ufaransa Kingsley Coman baada ya Bayern Munich kusema kwamba anaweza kuuzwa kwa bei ya £77m.

 

Kingsley Coman

Tottenham imemuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Wolves Nuno Espirito Santo kuwa mkufunzi mpya kwa kandarasi ya miaka miwili .

Manchester City ina mpango wa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa England Raheem Sterling kuhusu hatma yake , huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akiwa amesalia na miaka miwili katika kandarasi yake na mabingwa hao wa ligi ya Uingereza.

Rais wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi amechukua nafasi ya mkurugenzi wa michezo katika klabu hiyo Leonardo katika mazungumzo ya kumshawishi mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 inakamilika 2022.

Tetesi zinasema, Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich ana imani kwamba The Blues inaweza kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, mwisho wa msimu huu.

Mchezaji wa timu ya Portugal ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 Nuno Tavares, 21, atafanyiwa uchunguzi wa matibabu katika klabu ya Arsenal kabla ya kujiunga na The Gunners kwa dau la £7m kutoka Benfica.

Tetesi zinasema, Chelsea wamewasilisha ombi la mwisho kumsaini mshambuliaji wa Manchester United Lauren James, 19, dadake beki wa Blues Reece James.

Leicester inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan katika kinyang’aanyiro cha kumsaini winga wa Itali na Sassuolo Domenico Berardi, 26, ambaye amewavutia the Azzurri katika michuano ya 2020.

 

Newcastle United wamewasilisha ombi la £1.5m kumnunua beki wa Wolves Dion Sanderson huku wakishindana na Sunderland kumsaini mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 21.

Klabu ya RB Leipzig itamuwacha kiungo wa kati wa Austria Marcel Sabitzer kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu kwa bei ya chini huku Arsenal, AC Milan na Roma zote zikimuwania kiungo huyo mchezeshaji mwenye urmi wa miaka 27.

Nahodha wa klabu ya Rangers James Tavernier ananyatiwa na Manchester United, Brighton, Norwich na Arsenal. Mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 29 alitia saini kandarasi mpya mwezi Aprili , inayomfanya kusalia katika klabu hiyo hadi 2024.


KUSANYA PESA HAPA!

IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!Meridianbet

INGIA MCHEZONI

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.