Nyota wa Barcelona Antoine Griezmann ameripotiwa kuwa ameomba msamaha kwa mabosi wanaoifadhili Barcelona baada ya utani alioufanya uliotafsiriwa kama ubaguzi.
Griezmann na mwanatimu mwenzake Ousmane Dembéléwametokea katika video iliyozua utata ambayo walionekana wakiwatania wafanyakazi wa kijapani.
Kwa mujibu wa staa huyo, video hiyo ambayo ilivuma kwenye mitandao ya kijamii ilitafsiriwa vibaya kwa kuhusishwa na ubaguzi. Baada ya kuonekana kwa video hiyo Griezamann aliomba msamaha mapema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Alichapisha maneno yasemayo:
“Wakati wote nimekuwa kipaumbele kupambana na kila aina ya ubaguzi. Kwa siku za hivi karibuni, baadhi ya watu wameamua kunitangazia kile ambacho si mimi. Ninakanusha madai juu yangu na naomba msamaha ikiwa niliwaudhi marafiki zangu wa Japani”
Licha ya chapisho la Griezmann, Mkurugenzi wa Japonesse ambao ni miungoni mwa wafadhili wa Barcelona Rakuten, Hiroshi Mikitani naye pia alichapisha akidai kuwa atafuatilia kwa ukaribu zaidi kupata majibu kutoka klabuni hapo juu ya suala hilo.
Taarifa zingine zinasema kuwa Griezmann tayari pia amefanya mawasiliano na mkurugenzi huyo kuomba msamaha juu ya kilichotokea.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!


