Federico Chiesa Windoni na Bayern Munich

Meneja wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amempenda mshambuliaji wa Juventus Federico Chiesa, kwa mujubu wa vyanzo mbalimbali.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa  kwenye majukumu ya kitaifa na timu ya taifa ya talia ya Euro 2020, na kuonekana vyema kwenye fainali ya Jumapili dhidi ya England huko Wembley.

Chiesa alifunga mabao mawili dhidi ya Austria na Uhispania wakati wa hatua ya mtoano ya EURO 2020.

Windoni

Kwa mujibu wa chanzo cha habari cha Ujerumani, Nagelsmann angepeda kupata saini ya Chiesa, lakini amekiri kuwa pesa zinaweza kuwa shida.

Nyota huyo bado yupo kwa mkopo huko Juve kutoka Fiorentina, lakini Juventus ana kifungu cha kumnunua majira ya joto mwakani kwa ada ambayo inaweza kuongezeka hadi € 50m (£ 42.7m) na bonasi zinazohusiana na utendaji.

Msimu wa kwanza wa Chiesa huko Juventus ulimshuhudia akifunga mabao 14 na asisti 10 katika mechi 43 za mashindano yote, pamoja na mechi 16 kutoka michezo 30 ya Serie A.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.