Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amekemea vikali kitendo cha baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuwatumia kauli za kibaguzi wa wachezaji wa Uingereza Rashford, Sancho pamoja na Saka kwa kukosa penati katika mechi ya fainali jana.

Wachezaji hao vijana walichaguliwa kuwa miongoni mwa wapiga penati katika mechi ya kibabe ya fainali ambayo ilionekana kujawa na ufundi huku vijana wa Mancini, the Azurri wakionekana kuwa bora zaidi.

Goli la Luke Shaw dakika ya pili lilikaa mpaka kipindi cha pili dakika ya 67 ambapo beki wa kati Bonucci nae aliisawazisha Italy na kufanya ubao wa matokeo uwe 1-1 mpaka dakika tisini na zile za nyongeza katika fainali hiyo ya Euro 2020.

Wakati wa Penati wachezaji wa Uingereza lakini Kipa wa Italy Donnaruma ambaye ameibuka mchezaji bora wa michuano hii ya Euro 2020 aliokoa michomo ya Bukayo Saka na Jadon Sancho kabla ya Rashford kugonga mwamba.

Euro 2020

Kutokana na kitendo hicho wachezaji hawa watatu wameonekana kutumiwa jumbe za kejeli na kibaguzi za kutosha kutoka kwa mashabiki mbalimbali walioshabikia Uingereza na waziri mkuu Boris Johnson amepinga kitendo hicho.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa