Majira kama haya 2020, Antonio Rudiger alipewa jina la “Agent Rudiger”. Beki huyu alihusika sana kwenye mchakato wa Chelsea kumsajili Havertz na Werner.
Havertz na Werner ni wajerumani na Rudiger ni kama kaka yao kuanzia umri mpaka uzoefu na timu ya Taifa ya Ujerumani. Hakika beki huyu aliifanya kazi ya ziada kuisaidia Chelsea kuwavuta nyota hawa ambao walikuwa wakicheza Bundesliga.
Baada ya kutua kwenye EPL, kila mtu amekuwa na matokeo yake kwenye msimu wa kwanza. Safari hii, The Blues wanahusishwa na Antoinne Griezmann. Hapa lazima Thomas Tuchel angaalie tena, nani anamfaa katika kuhakikisha hili linatokea?
Si mwingine bali ni Kourt Zouma, Zouma na Griezmann wamecheza pamoja kwenye timu ya Taifa ya Ufaransa na wanafahamiana kwa ukaribu. Hii ni kusema kuwa ni zamu ya “Agent K” kuingia mawindoni katika harakati za kukamleta Griezmann kwa mkopo pale Stamford Bridge.

Griezmann anahusishwa na Chelsea ikiwa ni muendelezo wa Tuchel kutaka kuboresha kikosi kuelekea msimu ujao. Erling Haaland bado anamendewa kwa ukaribu na vigogo wa The Blues japokuwa BVB wamesema wazi – Hawamuuzi.
Upande wa pili, Barcelona wanahaha na hali mbaya ya uchumi klabuni hapo na hivyo, uwezekano wa kuwaachia baadhi ya nyota wake ni mkubwa ili waweze kufanya usajili na kuweka vitabu vyao vya benki katika hali iliyosawia.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!


