Baada ya kuripotiwa kuwa FA wamepigwa faini kwa makosa manne yaliyofanyika Wembley, Uefa imeanza uchunguzi wa matukio yote yaliyotokea kwenye Euro 2020 pale Wembley.
Mchezo wa fainali ya Euro 2020 kati ya Uingereza na Italia, uligubikwa na matukio ya vurugu kutoka kwa mashabiki. Baadhi ya malango ya kuingia uwanjani yalivunjwa, baadhi ya mashabiki kuumizwa, polisi na walinzi wengine kushindwa kukabiliana na vurugu za mashabiki n.k

Sambamba na kile kilichotokea nje ya uwanja, ndani ya uwanja kulikua na matukio ya kurushwa vitu mbalimbali wakati michezo ikiendelea, vurugu wakati wa nyimbo za taifa pamoja na kuwamulika wachezaji kwenye mchezo wa Uingereza vs Denmark.
Uefa imeamua kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya shirikisho la soka nchini Uingereza na hivyo uchunguzi wa matukio yote yaliyofanyika ndani na nje ya Wembley umeanza rasmi.
Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!


