Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Chelsea wanafanya mipango ya kumsajili Mfaransa Antoine Griezmann,30, kwa mkopo kutoka Barcelona.

Tottenham imemfanya mshambuliaji wa Southampton Danny Ings,28, kipaumbele chao wakiamini kuwa atacheza nafasi ya ushambuliaji sambamba na Harry Kane, wanayetaka kumbakisha.

Tetesi zinasema, Arsenal wana mpango wa kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves kwa kitita cha pauni milioni 35.

 

Mchezaji anayelengwa na washika bunduki Manuel Locatelli, 23, kiungo wa kati anayekipiga klabu ya Sassuolo na Italia, amekaribisha nia ya Juventus kumsajili.

Spurs na Manchester United zinataka kumsajili mlinzi wa Argentina Cristian Romero, 23, ambaye amefika nusu ya muda wa mkataba wake na Atlanta anakocheza kwa mkopo akitokea Juventus.

Tetetsi zinasema, Paris St-Germain wanajiandaa kutangaza usajili wa mlinda mlango wa AC Milan Muitaliano Gianluigi Donnarumma, 22.

Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Aston Villa na England Jack Grealish, 25, ameonywa dhidi ya kuhamia kwa mabingwa wa ligi ya Primia, Manchester City.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Winga wa England Andros Townsend, 29, anatafuta klabu mpya baada ya kukubali kuwa ana uwezekano wa kupewa mkataba mpya huko Crystal Palace.

Brentford wamejiunga na West Brom katika kinyang’anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Trevoh Chalobah. klabu ya Ufaransa ya Lorient pia inamtaka mchezaji huyo mwenye miaka 22.

Kiungo wa kati wa West Ham Felipe Anderson,28, yuko Italia kusajiliwa tena na Lazio-ikiwa ni miaka mitatu baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na Hammers.


JIUNGE NA FAMILIA YA MABINGWA!

Ndio, kama bado hujajiunga na Familia ya Mabingwa ya Meridianbet, huu ndio wakati wako! Tunakupatia Bonasi ya 3,500 Tsh papo hapo kama sehemu ya ukaribisho!

Italia, Italia Bingwa Euro 2020., Meridianbet

JIUNGE SASA!

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.