Wakati siku 10 za kupeperusha bendera za timu za Taifa zikifikia tamati, Mkurugenzi wa Shirikisho la Vilabu vya Ulaya, Charlie Marshall, aitaka Fifa kutoa tamko.
Vilabu vya Uingereza na nchi zingine za ulaya, vilipiga kura ya siri kukubaliana kutowaruhusu wachezaji kushiriki mechi za kimataifa kwenye nchi ambazo zipo kwenye orodha nyekundu (idadi kubwa au sehemu hatarishi kwa COVID19).
Katazo hilo ni matokeo ya utaratibu wa kukaa karantini kwa siku 10 kwa wasafiri wote wanaongia kwenye nchi za Ulaya wakitokea kwenye nchi hizo.
Marshall ameitaka Fifa kutoa tamko ndani ya saa 24 kuhusu hatma ya wachezaji wa Brazil ambao hawakuruhusiwa kushiriki mashindano hayo. Jumla ya wachezaji 6 kutoka EPL ni miongoni mwa wachezaji waliokua wameitwa kwenye kikosi cha Brazil na hawakuruhusiwa kushiriki.

Sheria ya Fifa inaruhusu wachezaji kufungukiwa kwa siku 5 endapo watashindwa kuzitumikia timu zao za taifa wakati ambao michezo ya Timu ya Taifa inafanyika. Kwa sababu hii, Wolves, Newcastle, Watford na Blackburn watawakosa baadhi ya wachezaji wao baada ya shirikisho la Soka nchini Chile, Mexico na Paraguay kulalamika wachezaji kutoruhusiwa kucheza michezo ya kufuzu Kombe la Dunia.
Liverpool, Man City, Man United, Chelsea, Leeds United na Everton zinasubiri tamko kama wanaruhusiwa kuwatumia wachezaji wa Brazil au hawaruhusiwi kuelekea muendelezo wa EPL.
Meridianbet inakuletea ushindi kwenye kiganjani kwako, unafurahia radha halisi ya burudani ya kasino mtandaoni na tabasamu la ushindi.



[email protected]
Nice update