Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Newcastle wanatarajiwa kumsajili mchezaji wa zamani wa Liverpool, kiungo wa kati Philippe Coutinho, 29 huku Barcelona wakitamani kumuuza mchezaji huyo.

Manchester United wanapanga kumfuatilia kiungo wa kati wa Monaco Mfaransa Aurelien Tchouameni, 21, huku wakiongeza kasi ya kutafuta mbadala wa nyota wa Ufaransa Paul Pogba, 28.

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe anaweza kutaka kipengele cha Olimpiki kiingizwe katika mkataba wowote unaowezekana na Real Madrid baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kueleza hadharani nia yake ya kuiwakilisha Ufaransa kwenye Michezo ya Paris mnamo 2024.

 

Tetesi za Soka Barani Ulaya.

Kocha wa Villrreal Unai Emery,50, ametupilia mbali ofa ya uhamisho kwenda Newcastle kwasababu klabu hiyo imetaka kiwepo kipengele kwenye mkataba wake kitakachowaruhusu kumtimua ikiwa watashuka daraja mwishoni mwa msimu.

Machester City wamemwambia kocha wa Leicester Brendan Rodgers,48, kuwa wangependa achukue mikoba ya Pep Guardiola Mhispania huyo mwenye miaka 50 atakapoachana na mabingwa hao wa ligi ya Primia.

Tetesi zinasema, Tottenham wanaongoza kinyang’anyiro cha kumnasa mhambuliaji wa Fiorentina Dusan Vlahovic, 21, huku Mserbia huyo akiwa tayari kuhamia ligi ya Primia.

Barcelona wana matumaini ya kumbakiza winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 24, kwa mkataba mpya wa miaka mitatu ifikapo mwishoni mwa Novemba.

 

Ousmane Dembele Anataka Kuendelea Kusalia Barca!
Osmane Dembele

Tetesi zinasema, Everton wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Real Mallorca na Ghana Iddrisu Baba, 25, mwezi Januari.

Barcelona watamsajili kiungo wa kati wa Tottenham mwenye umri wa miaka 24 Tanguy Ndombele mwezi Januari, lakini wanaweza tu kumudu mkataba wa mkopo kwa Mfaransa huyo.


MKWANJA WA KUSHATO NA AURORA BEAST HUNTER!

Mkwanja umetema ndani ya kasino za meridianbettz, Mchezo maridhawa wa Aurora Beast Hunter unakupa nafasi sawa ya ushindi leo hii, kila mzunguko una nafasi ya kuibuka mshindi, na mkwanja wako unaupata kila mzunguko utakapo kamilika.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.