Tetesi zinasema, Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard kwa £10m mwezi Januari.
Meneja mpya wa Barcelona, Xavi anataka klabu hiyo kumsajili tena kiungo wa kati wa Uhispania Thiago Alcantara, 30, kutoka Liverpool.
Tetesi zinasema, Barcelona wanafikiria kumsajili kwa mkopo winga wa kulia wa Chelsea na Marekani Christian Pulisic, 23.

Beki wa Manchester City na Uholanzi Nathan Ake, 26, analengwa sana na meneja mpya wa Newcastle Eddie Howe, ambaye hapo awali alikuwa meneja wa Ake huko Bournemouth.
Tetesi zinasema, Kiungo wa kati wa Leicester City na Nigeria Wilfred Ndidi, 24, na kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba wako kwenye rada za Real Madrid.
Tetesi zinasema, Chelsea na Real Madrid wanaweza kupambana katika kumnunua mchezaji wa Bayer Leverkusen na mchezaji wa Ujerumani Florian Wirtz, 18.
Chelsea inaandaa ofa ya kumnunua kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni, 21 pia wametuma dau la pauni milioni 34 kumnunua beki wa Real Madrid na Brazil, Eder Militao, 23.

Roma wapo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua beki wa pembeni wa Ureno Diogo Dalot, 22.
Leeds United imefanya mawasiliano na mshambuliaji wa Arsenal na England aliye chini ya umri wa miaka 21 Eddie Nketiah kuhusu kurejea Elland Road.
Tetesi zinasema meneja mpya wa Aston Villa, Steven Gerrard anataka kumsajili kiungo wa kati wa timu yake ya zamani, Rangers na Finland Glen Kamara, 26.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


