Messi Ndio Mchezaji Bora wa Muda Wote Duniani : Mwanasoka

Anaandika Deo Mwanasoka
Messi na mpira hawatengani Ndani ya Miguu yake mpira unapata hisia zote tano za fahamu. Achilia mbali mamlaka inayopokea kutoka katika ubongo wake.

Hayo hapo juu ni maelezo mafupi ya La Pulga Lionel Messi yaliyonijia harakaharaka baada ya kuitazama hii picha aliyopost brother kisha akaandika

“Hapo ndipo mwana wa Adam akapita na kuondoka zake” Nikaongeza comment kwamba “Na miguu yake itafanya njia pasipo na njia”

Nimeiona nikiwa juu ya kiti cha darasa nipo nyuma kabisa! Kama kawaida ‘back bench’ ni kwa ajili ya watukutu na watu wasiosikiliza darasani

Picha hii imeanza kwa kunishtua kisha ikayateka mawazo yangu na kunirudisha nyuma sana. Professor anaendelea kukokotoa hesabu zake kule mbele na mimi huku nyuma naendelea kuvuta kumbukumbu za Cuccitin Lionel Messi.

Kumbukumbu zangu zilianzia Paris kwenye ballon d’or za 2005. Gaucho alipokabidhiwa tuzo yake alisema “Hii tuzo inasema mimi ni bora zaidi duniani lakini nawaambia mimi sio bora hata ndani ya Barcelona”

Messi

mimi wala Sekamagenge Mwijuna tuliomuelewa Gaucho siku ile. Msururu wa wachezaji wote duniani hakuna aliyemsogelea Gaucho! Kivipi awepo aliyemzidi ndani ya Barcelona??Lakini Gaucho alimshatazama Lionel  wa miaka 16 na kuona kitu ambacho hata manabii wote dunia nzima hawakukiona. Ndani ya Messi alimuona Ronaldinho Gaucho na mchezaji mwingine juu yake.

Hapo ni kabla ya kuwafunga bao la karne Getafe. Unakumbuka anachukua mpira katikati ya uwanja kisha anawaacha wachezaji watano wa Getafe na kuwatungua kutoka kwenye angle ngumu??

Ni Messi huyu ambaye Giorgio Chiellini alisema njia pekee ya kumzuia ni kumuomba Mungu kabla ya mechi na kumtwanga buti mechi nzima. Licha ya hayo bado Messi amekatiza katikati ya Chiellini na kumlaza na viatu mara kadhaa.

Ni Lionel Messi huyu ambaye bado macho yangu yanasubiri kumshuhudia mchezaji bora kumzidi yeye. Subira ambayo ninafahamu haitakaa itimie.


WIKI NJEMA NA CRAZY TIME CASINO!

Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.