Goli kipa wa timu ya Chelsea Edouard Mendy ametumia mtandao wa kijamii leo, siku ya alhamisi kuwakosoa waandishi baada ya kutumia picha yake kimakosa katika habari ya beki wa Man City Benjamin Mendy.
Pia picha ya mchezaji wa Real Madrid Ferland imetumika kimakosa kwenye habari ya Benjamini Mendy ambayo inahusu tuhuma zake za ubakaji.

Eduoard na Ferland Mendy wote ni raia wa Senegali, na hawana uhusiano wowote na Benjamin ambaye ana uraia wa nchini Ufaransa.
“ni jambo linaoloumiza kuona mwaka 2021, nchini ufaransa na uingereza kwa kushindwa kutofautisha sio kwa majina wala sura, haya makosa ya picha inaonekana kwa majina lakini ni watu tofauti na sio kazi kuwatofautisha kwa sura, hususani wanapokuwa na jersey zao.”

Benjamin aliyeleta mzozo huo wa kuchanganya picha kwa sasa yupo rumande kwa mashitaka ya ubakaji na unyanyasaji wa kingono kwa mabinti sita.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


