Tetesi zinasema, Manchester United wanatazamiwa kushindana na Barcelona katika kutaka kumsajili winga wa RB Leipzig wa Kihispania Dani Olmo, 23.
Chelsea wanavutiwa na mlinzi wa Leicester City Wesley Fofana na wako mbele kidogo ya Manchester United katika kujaribu kumsajili beki huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20.
Tetesi zinasema, Barcelona wanapanga kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Hakim Ziyech lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Borussia Dortmund kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Morocco, 28.

Arsenal wako tayari kumpa mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette mkataba wa muda mfupi huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 akikaribia mwisho wa mkataba wake msimu ujao wa joto.
Villarreal wanapanga kukataa ofa zote kwa winga wa Uholanzi Arnaut Danjuma mwezi Januari, huku Liverpool wakimfuatilia mshambuliaji huyo wa zamani wa Bournemouth, 24.
Manchester United wameanza mipango ya mrithi wao kuchukua nafasi ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, huku Brendan Rodgers wa Leicester City akiwa mgombea wanayempendelea zaidi
Tetesi zinasema, Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane amejibu maombi ya Manchester United kwa kusema atapatikana mwishoni mwa msimu huu.
Kocha mpya wa Barcelona Xavi anataka kumbakisha mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele lakini amemwambia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aamue hatma yake sasa.

Mlinda mlango wa Ujerumani Manuel Neuer ameanza mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba wake na Bayern Munich na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 anataka mkataba wa hadi angalau mwaka 2025.
Tetesi zinasema Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 32, atakuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu kutokana na jeraha la mguu baada ya kujiunga na Wales wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Unasababu milioni za kucheza unavyotaka ukiwa na mabingwa meridianbet, lakini unasababu moja ya kushinda mamilioni katika kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo maridhawa wa Crazy Time unakupa sababu hizo kuwa mmoja wa washindi leo hii.


