Wakati dunia ikiamini kuwa Manchester United inafanya mipango ya kumpa ajira Zinedine Zidane kuwa kocha wa timu hiyo, inadaiwa staa wa timu, Cristiano Ronaldo anapendekeza jina la kocha mwingine kabisa.

Ronaldo amempendekeza Luis Enrique ambaye amewahi kuwa kocha wa Barcelona.
Ronaldo anataka Luis Enrique ndiye awe mrithi wa Solskjaer badala ya Zidane ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja na kwa mafanikio makubwa Real Madrid.

Makocha wengine wanaotajwa kuwa wanaweza kupata nafasi ya kuinoa Man ni Erik ten Hag wa Ajax, Mauricio Pochettino wa Paris Saint-Germain na Brendan Rodgers wa Leicester City.
Enrique amekuwa akiinoa Hispania tangu mwaka 2019, kocha huyo mwenye umri wa miaka 51 aliifundisha Barcelona kwa mafanikio makubwa akibeba LaLiga mara mbili na Champions League mara moja.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


