Eden Hazard Kurejea Chelsea kwa Mkopo?

Klabu ya Chelsea inaripotiwa kuwa inafikiria kumrejesha Eden Hazard katika klabu hiyo kwa mkataba wa mkopo.

Winga huyo wa Ubelgiji aliondoka Chelsea na kuungana na Real Madrid mwaka 2019 baada ya miaka minane na The Blues, lakini amekuwa na changamoto za majeraha tangu alipowasili Uhispania.

Hazard amekabiliwa na changamoto ya majeraha na hajafanikiwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, jambo ambalo limesababisha tetesi kibao juu ya mustakabali wake klabuni hapo.

Eden Hazard
Eden Hazard alikuwa kwenye fomu nzuri alipokuwa Chelsea.

Real Madrid sasa wanataka kumuuza, kwa mujibu wa ABC, klabu hiyo ya Uhispania inalenga kumuuza nahodha huyo wa Ubelgiji kwenye soko la usajili la majira ya kiangazi.

Ripoti hiyo pia inaongeza kuwa hii inaweza kumfungulia Hazard milango ya kurejea London, wakati The Blues wakitajwa kuwa wanafikiria mkataba wa mkopo kupitia dirisha la mwezi Januari, huku chaguo la kumnunua mwishoni mwa msimu kuwa kwenye mpango huo.

Eden Hazard alicheza mechi 352 wakati akiwa na Chelsea, akiifungia klabu hiyo mabao 110 katika kwa kipindi hicho chote.


PANDISHA THAMANI YA DAU LAKO NA FAI CAI SHEN

Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.