Winga huyo wa Ubelgiji aliondoka Chelsea na kuungana na Real Madrid mwaka 2019 baada ya miaka minane na The Blues, lakini amekuwa na changamoto za majeraha tangu alipowasili Uhispania.
Hazard amekabiliwa na changamoto ya majeraha na hajafanikiwa kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha kwanza, jambo ambalo limesababisha tetesi kibao juu ya mustakabali wake klabuni hapo.

Real Madrid sasa wanataka kumuuza, kwa mujibu wa ABC, klabu hiyo ya Uhispania inalenga kumuuza nahodha huyo wa Ubelgiji kwenye soko la usajili la majira ya kiangazi.
Ripoti hiyo pia inaongeza kuwa hii inaweza kumfungulia Hazard milango ya kurejea London, wakati The Blues wakitajwa kuwa wanafikiria mkataba wa mkopo kupitia dirisha la mwezi Januari, huku chaguo la kumnunua mwishoni mwa msimu kuwa kwenye mpango huo.
Eden Hazard alicheza mechi 352 wakati akiwa na Chelsea, akiifungia klabu hiyo mabao 110 katika kwa kipindi hicho chote.
Wiki nyingine ya kushinda mamilioni ukiwa na kasino maridhawa za meridianbettz. Mchezo pendwa wa Fai Cai Shen unakupa thamani ya dau lako, kwa kiasi kidogo cha dau unaweza kushinda mkwanja mrefu.


