John McGinn Mrithi Sahihi wa Pogba?

Kiungo wa kati wa Aston Villa John McGinn ameripotiwa kuibuka kama mbadala wa Paul Pogba kwa Manchester United. 

Pogba anakaribia miezi sita ya mwisho ya mkataba wake Old Trafford na anaweza kuanza mazungumzo na vilabu kwingine kuanzia mwezi Januari na kuendelea.

Ujio wa Ralf Rangnick unadaiwa kumfanya Pogba kufikiria kusaini mkataba mpya United, lakini nia yake bado haijawa wazi huku hali ya mkataba wake ikiwa bado tata.

John McGinn Mrithi Sahihi wa Pogba?
John McGinn

Kwa mujibu The Sun, Rangnick anaamini kwamba McGinn angelingana na mtindo wa uchezaji anaotaka kuutumia akiwa United na anaweza kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Scotland iwapo Pogba ataondoka.

Ripoti hiyo inaongeza kuwa Villa itadai zaidi ya pauni milioni 50 kwa ajili ya biashara hiyo, ingawa, mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 bado unadumu 2025.

McGinn ana mabao matatu na asisti moja kwenye mechi 13 za Premier League msimu huu na amefunga jumla ya mabao 16 na asisti 20 kwenye michezo 124 alizoichezea Villa tangu alipowasili mwaka 2018.

United wanadaiwa kukaribia kusajili kwa mara ya kwanza chini ya Rangnick, ingawa, huku dili la Amadou Haidara wa RB Leipzig likidaiwa tayari wamekamilisha makubaliano, ni suala la muda tu.


 

MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.