Klabu ya Bayern Munich imethibitisha kuwa mchezaji wake Joshua Kimmich hatakuwepo kwenye kikosi mpaka mwaka 2022 kutokana na tatizo la mapafu baada ya kupatikana na maambukizi ya korona wiki mbili zilizopita.
Joshua alijitenga kwa muda wiki mbili ambapo siku ya mwisho ilikuwa ni tarehe 8 ya Jumatano mwezi disemba lakini bado hali yake haijatengemaa kuweza kurudi uwanjani, kimmich alithibitisha habari kutokuwepo kikosini mpaka mwishoni mwa majira ya baridi.

“Nina furaha kuwa karantini iliyosababishwa na korona ambayo imekwisha sasa, naendelea vizuri, ila siwezi kufanya mazoezi kutokana na tatizo la mapafu ila nitakuwa nafanya mazoezi na nina shauku kubwa ya kurudi tena uwanjani mwezi January.” Alimesema Joshua Kimmich
Joshua mwezi wa Oktoba aliteka vichwa vya vyombo vya habari baada ya kuthibitsha kuwa hakuchanja chanjo ya korona kutokana na mtazamo wake, huku akiwakosoa watalaamu wa afya na baadhi ya wahamasishaji, huku akisisitiza kuwa yeye sio mpinga chanjo.
Unaweza kujishindia mamilioni katika kasino yako pendwa ya meridianbettz, mchezo wa Agent Jane Blonde Return ni moja ya michezo inayopendwa kwasasa huku ikiwafanya wachezaji kuwa mamilionea kila siku. Unasubiri nini! ungana na Agent Jane Blonde akufanye milionea.
CHEZA HAPA


