Man United Hali Si Shwari vs Rangnick.

Anafahamika kama muasisi wa “gegenpressing”, Ralf Rangnick anakalia koti kavu pale Man United. Hali sio shwari!!

Kiuhalisia, mabadiliko ndani ya Man United ni madogo sana au pengine hayapo kabisa. Maisha chini ya Ole Gunnar Solskjaer na sasa hivi chini ya Ralf Rangnick, tofauti hakuna.

United wanacheza katika namna ambayo haiwavutii mashabiki wengi wa timu hiyo. Matokeo yao uwanjani ni tia maji tia maji, wengine wanaenda mbali zaidi, unaambiwa, uwepo wa CR7 umeharibu viwango vya wachezaji wengi.

Wapo wanaouliza, ni kweli kulikuwa na mpango wa kumsajili CR7 au Man United walikurupuka tu kwa misingi ya kibiashara? Nafasi yake ni ipi hasa? Toka amerejea Old Trafford, wachezaji wamegawanyika, wapo wanaoungana nae na wapo wanaomuogopa. Maelewano yake na wachezaji wenzake sio mazuri kama inavyoonekana kwenye kideo. Kulikoni?

Cristiano Ronaldo

Inasemekana, hali ya hewa sio shwari miongoni mwa wachezaji wa United. Takribani wachezaji 11 wanataka kuondoka klabuni hapo kutokana na mazingira yaliopo kwa sasa ambayo wengine wamekuwa nayo kwa muda mrefu. Baadhi ya wachezaji hawapendezwi na kile anachokifanya Rangnick na benchi lake la ufundi. Inasemekana, Ralf anawapigisha wachezaji mzigo mzito kuliko uwezo wao huku, wengi wakiwa hawaelew muelekeo wa timu chini ya Rangnick.

Mpasuko uliopo ndani ya klabu unatoa matokeo halisi ya kile wanachokifanya uwanjani. Endapo hali itaendelea kuwa hivi, pengine tutegemee msimu mbaya zaidi kwenye historia ya The Red Devils.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.