Tetesi za Soka Barani Ulaya.

 

Tetesi zinasema, Mshambuliaji wa Paris St-Germain, Kylian Mbappe, 23, bado anaweza kukataa kuhamia Real Madrid na kusaini mkataba mpya na klabu yake.

Tetesi zinasema kiungo wa Spurs, Tanguy Ndombele, kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25, ana matumaini ya kuondoka Tottenham Hotspur mwezi huu.

Winga wa Uholanzi Steven Bergwijn anaonekana kukaribia kuondoka Spurs, huku Ajax ikiwa miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

 

Tetesi zinasema, mshambuliaji wa Bayer Leverkusen na Jamhuri ya Czech Patrik Schick, 25, anasema ana furaha katika klabu hiyo ya Bundesliga licha ya uvumi kuhusu kuhama mwezi Januari.

Aston Villa wako katika mazungumzo ya juu zaidi kumnunua Lucas Digne kutoka Everton, huku beki huyo wa kushoto wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 akiaminika kupendelea kuhamia kikosi cha Steven Gerrard.

Tetesi zinasema, Newcastle United wamewasiliana na Burnley kumnunua mshambuliaji wa New Zealand Chris Wood, 30.

 

Kipa wa zamani wa Newcastle, Shay Given amemshauri mwenzake Caoimhin Kelleher, 23, kuondoka Liverpool katika dirisha la uhamisho la mwezi huu ili kipa huyo wa Jamhuri ya Ireland apate muda zaidi wa kucheza.

Beki wa Arsenal, Sead Kolasinac amefanya mazungumzo na Marseille kuhusu uhamisho wa bila malipo msimu wa joto, huku beki huyo wa kushoto wa Bosnia, 28, akiwa hana nafasi kwenye Uwanja wa Emirates.

Tetesi iznasema, Kocha mkuu wa Chelsea, Thomas Tuchel amependekeza kiungo wa kati wa Uingereza Ross Barkley, 28, anaweza kuruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo mwezi huu.


Jiachie na Almighty Aztec

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

Cheza Hapa

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.