Usajili Wa Aubameyang, Kizungumkuti.

Yamesalia masaa 6 kabla dirisha la usajili mdogo kufungwa barani Ulaya. Pierre-Emerick Aubameyang bado hakijaeleweka. Ni kizungumkuti.

Wakati inaripotiwa kuwa FC Barcelona na Juventus zimeonesha nia ya kutaka kumsajili Aubamayeng, ni Barca ndio walioenda mbali zaidi na kuanza mazunguzo na Arsenal kuhusu uwezekano wa usajili wa mchezaji huyo.

Sehemu kubwa ya majadiliano baina ya timu hizi, zilikuwa ni mkataba wa mkopo wa miezi 6 lakini, kipengele kikubwa ni nani atalipa mshahara wa nyota huyo (£350,000 kwa wiki)?

Barca wanahali mbaya kiuchumi, Ousmane Dembele amegoma kusaini mkataba mpya na japokuwa klabu inamlamzimisha kuondoka kabla ya dirisha hili kufungwa, kuna kila dalili Dembele atabaki Cam Nou mpaka mwisho wa msimu atakapomaliza mkataba wake.

Kubaki kwa Dembele na kumsajili Aubamayeng ni kizungumkuti. Barca hawana pesa ya kuwalipa mishahara wachezaji wote wawili. Lazima wauze ndio wasajili na hata hivyo, bado Aubameyang atatakiwa kupunguza mshahara wake maradufu ili kukamilisha usajili kule Barcelona.

Kwa sasa, Aubameyang yupo nchini Uhispania jambo ambalo hata viongozi wa Arsenal wanashangaa imewezekanaje yeye kwenda nchini humo wakati huu ambao, Barca na Arsenal hawajafikia makubaliano yeyote ya mchezaji huyo kuondoka Emirate leo?

Uhondo unanoga zaidi sasa hivi ambapo, inaripotiwa kuwa, mazungumzo kati ya Barca na The Gunners yamesitishwa kutokana na kutokua na muafaka wa nani atalipa mshahara wa Aubameyang. Kwa hali hii, Pierre atarudi Uingereza muda wowote kuanzia sasa.


VUNA MKWANJA NA KENO

Dakika tano pekee zinakutosha kuwa mmoja wa washindi wa mkwanja mrefu ndani ya kasino pendwa ya meridianbettz katika sloti maridhawa ya KENO, moja ya michezo inayoipa thamani dau lako.

tetesi, Tetesi za Soka barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.