Beki wa Manchester City, Ruben Dias, 24 anatarajiwa kuendelea kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita zaidi baada ya kupata majeraha ya nyama za paja.

Mpaka sasa, Dias amekosa mechi tatu pekee kati ya mechi 28 ambazo klabu ya Manchester City imecheza katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).
“Ni mchezaji muhimu ambaye tukakosa huduma zake. Upekee wa mchango wake ni miongoni mwa sababu ambazo zimetudumisha kileleni mwa jedwali la EPL kwa kipindi kirefu,” alisema kocha Pep Guardiola.
Dias sasa anatarajiwa kukosa mechi tano zijazo za Manchester City ambazo watacheza dhidi ya Sporting CP (UCL), Crystal Palace, Southampton, Burnley na Liverpool mtawaliwa.
Dias alijiunga na Manchester City akitokea Benfica ya Ureno kwa dau la €68M mnamo Septemba 2020. Tangu wakati huo, amesaidia City kushinda mechi 26 kati ya 57 bila kufungwa na kuwaongoza kunyanyua taji la EPL na Carabao Cup mnamo 2020-21.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


