Neymara anasema safari ya leo kwenda Real Madrid sio safari ya kitoto. Anatambua vyema mchaka mchaka wanaoenda kukutana nao, lakini anasema wao ni wanasoka, na wanaishi kwa sababu ya safari kama ya leo.
Neymar anasema nyakati kama hizi za kukutana na wahasimu wenye ushindani mkubwa huja mara moja moja katika maisha, na wanapaswa kucheza soka na kufurahia nyakati hizo fursa inapokuwepo.

Katika mazungumzo yake na Diario Sports, Neymar amesisitiza kuwa analifahamu vyema sana dimba la Santiago Bernabeu, baada ya kutumia miaka yake minne kuichezea klabu ya Barcelona -mhasimu wakubwa wa Real huko Hispania.
“Itakuwa mechi nzuri, Naujua uwanja vizuri na tunajua kitakachotokea, kwamba tutakuwa kwenye presha kubwa, lakini sisi ni wachezaji ambao tumezoea kucheza nao. Tunapaswa kucheza mchezo wetu, kuwa na furaha, kufurahia maisha ya soka letu. Kwa sababu nyakati hizi hutokea mara moja tu.”
– Neymar
PSG wanavaana na Real wakiwa na ahueni ya ushindi uliopita wa goli 1-0 waliopata dakika za lala salama, ahsante kwa kinda wao Kylian Mbappe! Leo mziki utakuwa mnene sana ugenini, na PSG wanahitaji kuweka ngucu ya ziada kuhakikisha wanaondoka na ushindi.
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


