Raisi wa klabu ya PSG Al-Khelaifi na mkuregenzi wake Leonardo wafikishwa kamati ya maadili na nidhamu ya UEFA kwa uchunguzi kwa kufanya fujo na kuingia kwenye vyumba vya waamuzi vya kubadilishia nguo pasipo utaratibu.
Vyanzo vinathibitisha kuwa Nasser Al-Khelaifi na Leonardo walishuka chini kotoka kwenye sehemu zao baada ya mchezo kuisha, na kwenda kwenye vyumba vya waamuzi na kuanza kulalamikia maamuzi yao kwenye mchezo ambao walipoteza kwa goli tatu 3-1.

“Utaratibu umejikita zaidi kwenye kanuni za UEFA ambazo zinahusu msingi mzima wa uendeshaji pia tabia zisizo sahihi za wachezaji na wasimamizi.” Msemaji UEFA alinukuliwa.
Malalamiko yao makubwa yalikuwa kuhusu goli la kwanza ambalo alifunga mshambuliaji Karim Benzema, kuwa kipa Gianluigi Donnarumma alifanyiwa madhambi na ilipaswa apewe free kick.
Kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettino kwenye kikao na waandishi baada mechi kuisha alinukuliwa akisema, “ilikuwa faulo ya wazi na niliwaacha wachezaji wajisikie ile hali ya kutotendewa haki.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


