Kocha mkuu wa klabu Newcastle Eddie Howe anaamini kuwa Chelsea itakuwa imara uwanjani licha ya kuwekewa vikwazo na serikali ya Uingereza kutokana na mmiliki wa klabu hiyo kuhusishwa kuwa na ukaribu na raisi wa Urusi.
Eddie Howe ambaye amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi February kwenye ligi kuu ya Uingereza na kutangazwa leo ijumaa, anatarajia kuiona Chelsea ikimaliza nafasi tatu za juu.

“Sidhani kama Chelsea itaathilika kwenye upande wa uchezaji,” alisema kocha huyo wa Newcastle, ambapo timu yake imecheza michezo tisa bila ya kupoteza huku wakipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Southampton siku ya jana alhamisi.
“Kwetu sisi, huwezi kubadili maandalizi yetu kivyovyote. Nitakuwa nawaangalia Chelsea kihistoria na kujaribu kutengeneza mpango mkakati wa mchezo na kuajaribu kwenda kushinda.
“Sitaraji chochote uwanjani, kiukweli, kuwa na tofauti yeyote.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


