Golikipa wa timu ya PSG Gianluigi Donnarumma amekosolewa vikli na vyombo vya habari nchini Ufaransa baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya siku ya jumatano dhidi ya Rea Madrid kwenye dimba la Santiago Bernabeu.
Golikipa huyo kutoka nchini Italia Donnarumma alizidiwa nguvu na mshambuliaji wa Madrid Benzema kabla ya kufunga goli lake la kwanza, baadaya kupatikana kwa goli hilo PSG walishuka hamasa na kurushu goli zingine mbili na kuondolewa kwenye michuano hiyo.

Donnarumma alichapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiomba msamaha, “kuondolewa kwenye klabu bingwa ulaya, ni jambo zito, siku kazaa nyuma hazikuwa rahisi lakini kutoka kwenye hichi kipindi kigumu tutakuwa imara.
“Sasa kitu tunachoweza kufanya ni kufikilia kuhusu sasa, kushinda ligi na kutoa kila tulichonacho, kama ninavyofanyaga siku zote, kwa ajiri ya nembo hii, klabu hii na mashabiki wetu, tuanze upya kwa pamoja.”
Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000 katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.


