Raja Casablanca Yamtungua Vipers Vibaya Sana

Michuano ya klabu bingwa barani Afrika ilianza hapo jana ambapo kundi ambalo yupo Simba ya Tanzania ndilo kundi ambalo yupo Raja Casablanca na mechi ya jana amembugiza Vipers kipigo cha mbwa mwizi.

 

Raja Casablanca Yamtungua Vipers Vibaya Sana

Vipers amekufa ugenini kwa mabao 5-0 huku mlinda mlango wao akifanya makosa kadha wa kadha ambayo yameigharimu timu hivyo kusababisha timu hiyo kufungwa kwa fedheha ugenini.

Mpaka kufikia dakika 45 za kipindi cha kwanza, Vipers walikuwa tayari wamefungwa mabao 3 kwa bila huku bao la mapema zaidi likifungwa dakika ya mapema kabisa ya mchezo ambayo ni dakika ya 5.

Raja Casablanca Yamtungua Vipers Vibaya Sana

Raja Casablanca kwasasa ndiye anayeongoza kundi hilo akiwa na pointi tatu na mabao matano huku akisubiri mechi ya pili ya leo kati ya Simba dhidi ya Horoya itakayopigwa majira ya saa 1:00 usiku.

Baaada ya hapo Raja mechi inayofuata atamenyana dhidi ya Simba 18 Februari katika dimba la Mkapa.

Acha ujumbe