Klabu ya Morocco, Raja Casablanca imefanikiwa kuchukua kombe la shirikisho Afrika baada ya kufunga magoli 2-1 dhidi ya Js Kabylie FC ya Algeria.
Magoli mawili kutoka kwa Sofiane Rahimi na Ben Malango raia wa Congo DRC yalitosha kabisa kuweka msumari wa moto kwa timu ya JS Kabylie.
JS Kabylie walifanikiwa kuingia katika fainali ya michuano Kutokana kwa mara ya kwanza toka mwaka 2002 lakini bahati haikuwa kwao kutokana na ubora mkubwa uliooneshwa na timu ya Raja kutoka huko Morocco.
Kutokana na ushindi huo, hivi sasa ni rasmi Raja ambao ni mabingwa wa kihistoria kutoka Morocco wamefanikiwa kuongeza idadi ya makombe ya Afrika mara sita. Makombe mengine ni lile la CAF Champions League ambalo wamechukua mara tatu na hili sasa wamechukua mara tatu tayari mpaka sasa.
Itakumbukwa pia timu hii ilikuwa na wachezaji 10 uwanjani kutokana na mchezaji wao Voctor Gomes kutolewa nje kwa kadi nyekundu kutokana na mchezo wa hatari aliomchezea mchezaji wa JS Kabylie lakini idadi hii haikuwafanya wakubali kufungwa!
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

