Lautaro Amaliza Msimu Kwa Kubeba Copa America

Bao la nahodha wa Inter Lautaro Martinez liliiwezesha Argentina kushinda Fainali ya Copa America dhidi ya Colombia na kumsaidia kuwa mfungaji bora wa mashindano hayo.

 Lautaro Amaliza Msimu Kwa Kubeba Copa America
Argentina ya Lautaro Martinez ilishinda Copa America kwa mara ya pili kutokana na bao katika muda wa ziada kutoka kwa nahodha huyo wa Inter.

Pia meridianbet inatoa michezo ya kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, poker, Roullette, sloti na mingine kibao. Ingia meridianbet na ucheze sasa.

Hii ina maana kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 sio tu alinyanyua kombe hilo akiwa na timu yake ya taifa bali pia alikuwa mfungaji bora wa mashindano hayo, akiwa amefunga mabao matano ndani ya dakika 221.

 Lautaro Amaliza Msimu Kwa Kubeba Copa America

Ushindi wa Lautaro na Argentina ulikuja miezi michache tu baada ya ushindi wa Inter wa Serie A, uliochochewa na El Toro, mfungaji bora wa ligi mnamo 2023-24 akiwa na mabao 24.

Mkataba wa Martinez huko Stadio Meazza unamalizika Juni 2026, lakini hivi karibuni atasaini mkataba mpya na wababe hao wa Serie A kama ilivyotangazwa tayari na wakala wake na rais wa Nerazzurri Beppe Marotta.

Mchezaji huyo alijiunga na Inter mnamo 2018 kutoka Racing Club na amefunga mabao 103 ya Serie A katika mechi 206.

Acha ujumbe