Liverpool Wanamtupia Macho Arnaut Danjuma

Liverpool wanatajwa kuwa na nia ya kumnunua nyota wa Villarreal Arnaut Danjuma.

Danjuma amejiunga na Villareal hivi karibuni, akiwasili klabuni hapo kama usajili wa pili gharama zaidi wa klabu wa wakati wote wa majira ya joto.

Winga huyo alijiunga kwa kitita cha euro milioni 23.5 kutoka Bournemouth na amekuwa akifanya vizuri na kuwavutia vilabu vingine tangu wakati huo, akiwapa Villarreal walichotarajia kutoka kwake.

Danjuma tayari amefunga magoli saba na kutoa asisti mbili katika mechi zake 15 za kwanza akiwa na Villarreal, lakini hilo limemfanya avutie na vilabu vingine.

Liverpool Wanamtupia Macho Arnaut Danjuma

Kwa mujibu wa Sport, Liverpool sasa wanamtolea macho nyota huyu wa Uholanzi huku Jurgen Klopp akitajwa kuwa shabiki wake mkubwa.

Klopp atawapoteza Mo Salah na Sadio Mane kwa mwezi ujao, wakati Kombe la Mataifa ya Afrika litakapoanza, na hilo linaweza kumshawishi kumfukuzia Danjuma Januari.

Villarreal hawana uwezekano wa kuachana na nyota wao mpya kirahisi, kwa hivyo Liverpool italazimika kulipa zaidi takribani €23.5m uwezekano wa kumpata Danjuma.

Hii itawapa Villarreal nafasi ya kupata faida kwa mchezaji huyo, ingawa iko wazi wangependa Danjuma kuendelea kuwepo zaidi ya mwezi Januari.


 

NJIA RAHISI YA MKWANJA NA TITAN DICE

Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

Acha ujumbe