Shirikisho la Soka la Nchini Zambia (FAZ) limefanya mabadiliko ya benchi la ufundi wa timu ya taifa, kuteua kocha mwenye uzoefu George Lwandamina kuwa kocha wa muda wa Chipolopolo, akichukua nafasi ya Moses Sichone. Mabadiliko haya yametangazwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa shirikisho hilo FAZ, Iva Lengwe.

Lwandamina atasaidiwa na kocha wa Power Dynamos FC Oswald Mutapa Jr huku FAZ ikibainisha kuwa mabadiliko haya yanahusiana na nafasi ya kocha mkuu na msaidizi wake wa kwanza pekee. Nafasi zingine za benchi la ufundi hazibadiliki na zitaendelea na majukumu yao.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Mabadiliko haya yametokea baada ya Sichone na msaidizi wake wa zamani Perry Mutapa kuachishwa nafasi zao kufuatia matokeo ya AFCON 2025. FAZ imeeleza kuwa hatua hizi zinachukua nguvu mara moja ili kuhakikisha mpango wa mafunzo na maandalizi unaendelea bila ucheleweshaji.

Kazi ya kwanza ya Lwandamina itakuwa kuiongoza Zambia kwenye Four-Nation Tournament itakayofanyika Francistown, Botswana, kuanzia Machi 23 hadi 31, 2026. Taarifa zinaeleza kuwa mabadiliko haya yametolewa kwa nia ya kuhakikisha timu inakuwa imara na tayari kwa mashindano makubwa ya kimataifa.


