Euro 2020: Ramsdale Mbadala wa Henderson

Aaron Ramsdale amechukua nafasi ya golikipa wa Man United na Timu ya Taifa ya Uingereza – Dean Henderson katika muendelezo wa Euro 2020.

Henderson alipata majeruhi ya paja ambayo yanaendelea kumueka nje ya uwanja na hajaungana na wachezaji wenzake wa Uingereza kwenye vipindi vya mazoezi ya timu hiyo.

Kwa mujibu wa taratibu za Uefa, timu zinaruhusiwa kubadilisha golikipa kwa sababu za kiafya muda wowote wa mashindano.

Kuondolewa kwa Henderson kwenye kikosi cha Uingereza kinachocheza Euro 2020, kunamrudisha kipa huyo kwenye klabu yake (Man United) kwa ajili ya matibabu zaidi kuelekea kuanza kwa msimu wa EPL, 2021/22.

Ramsdale alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Uingereza waliocheza michezo ya kirafiki mapema mwezi huu na sasa atafanyiwa vipimo kadhaa vya Covid19 kabla ya kujiunga rasmi na timu hiyo.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

3 Komentara

    Anafaa yuko vizuri

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.