Lando Norris Asaini Mkataba Mpya McLaren.

Devera kinda wa timu ya McLaren, Lando Norris amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo. 

Norris alianza kuitumikia timu hiyo kwenye F1 mwaka 2019 na huu ni msimu wake wa 3 kunako mashindano ya F1. Kwa msimu huu pekee, Lando Norris ameshika nafasi 4 katika mbio 4 alizocheza akiwa na McLaren.

Japokuwa muda wa mkataba mpya haujawekwa wazi, McLaren wamethibitisha dereva mwenza wa Norris, Daniel Ricciardo ambaye pia ni bingwa mara 7 wa Grand Pix, ataendelea kuwepo kwenye timu hiyo mpaka zaidi ya mwaka 2022 ikiwa ndio kwanza anauanza mkataba wake wa miaka 3 msimu huu.

Lando Norris

Mkurugenzi wa timu ya McLaren, Zak Brown amenukuliwa akisema “nimefurahi kuongeza makubaliano yetu na Lando kwa zaidi ya 2022. Amekuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya timu yetu na ameongeza ukuaji wake tangu alipoanza kuwa nasi mwaka 2017.

Lando ni miongoni mwa vipaji vikubwa kwenye F1 na tunatazamia kuendelea kumuona akiongeza kiwango na ubora wake ndani na nje ya uwanja.”


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

BASHIRI SASA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.