KMC FC Yaendeleza Makali Yake

Klabu ya KMC FC ambayo ipo chini ya kocha mkuu Thiery Hitimana imepata ushindi wake Wa pili mfululizo baada ya kuitandika Azam FC kwa mabao 2-1.

Kmc ndio waliotangulia kupachika bao kupitia kwa mchezaji Wao na baadae bao hilo kusawazishwa kupitia kwa Nzigamasabo Steve hivyo kwenda mapumziko ubao ukisomeka 1-1.

Baada ya kwenda kupata nasaha kwa mako ha  wao, timu zilirejea uwanjani kwaajili ya kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili ambapo Kmc walionekana kuutawala mchezo ndipo wakafanikiwa kupata bao LA kuongoza kupitia kwa George Makang’a.

Golikipa wa Kmc David mapigano amekuwa na mchango mkubwa Sana kwenye hizi alama Tatu ambazo wamezipata kutokana na kuokoa mipira ya hatari iliyokuwa ikilenga lango Lao na kuifanya timu ipande hadi nafasi ya Tatu baada ya kufikisha point 13.

Afisa Habari Wa Wanakinoboys, Christina Mwagala alisema: “Timu ilikuwa imejiandaa vizuri kimwili na kiakili kwenye huu mchezo kwani point 3 ndizo zilikuwa muhimu kwao, Lakini pia hakusita kuwashukuru mashabiki waliojitolea Leo kufika uwanjani kwaajili ya kuisapoti timu Yao.”

Mechi ijayo KMC watavaana na mabingwa Wa kihistoria Young Africans (Yanga) ambao wapo nafasi ya pili kwenye msimamo,  sio mchezo rahisi kwa timu zote mbili kutokana na Yanga kuwa bora hivi karibuni Lakini pia vijana wa Thierry Hitimana wanaimarika kwani wamechukua point 3 kwa Azam na pointi 1.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa tarehe 26 baada ya Yanga kucheza dhidi ya Simba siku ya Jumapili.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.