Meridianbet imeendelea na zoezi la kumtafuta bingwa wa Danadana kwenye maduka yote ya kampuni ya Meridianbet, na leo zoezi hilo lilifanyika kwenye maduka mawaili, maeneo ya Kariakoo na Karume.

Mapema sana timu ya masoko iliyoongozwa na Meneja Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya Meridianbet Bw Matina Nkurlu, ilifika duka la kwanza la Max 75 linalopatikana Kariakoo nyuma ya kituo cha daladala zinazokwenda Mbagala au Buza, wadau wengi walijitokeza kushiriki shindano hilo, ila kanuni ni lazima apatikane bingwa wa duka ambaye ni mfalme wa wote.

 

DANADANA

Mshindi alipatikana kwa mbinde sana, baada ya kuchuana na wenzake saba, ila alifanikiwa kuwashinda wote, namtambilisha kwenu Mfalme na Bingwa wa Danadana wa duka la Max 75 kuwa ni Japhet Joel aliyecheza tiketi ya 1000/= na kujinyakulia zawadi ya Mpira mpyaa na Fulana kalii kutoka Meridianbet.

Haikuishia hapo Shindano hilo liliendelea kwenye duka la Max 80 lililopo Karume karibu na Kituo cha Daladala cha magari yanayoelekea Kigamboni na Gongolamboto.

 

DANADANA

Mshindi wa duka hilo alikuwa ni Frank Hasani ambaye alishindana vikali na wamba wengine hususani kijana mmoja mwenye kipaji kikubwa cha kupiga danadana, Omary Awadhi.

Shindano la Bingwa wa Danadana bado linaendelea ambapo litahusisha maduka yote ya Meridianbet yaliyopo mkoa wa Dar ES Salaam, ambapo kila duka litatoa mshindi mmoja na baadae washindi wote watajumuishwa kwenye Fainali yenye zawadi NONO.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa