Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa amelalamikia pelnati ya mchezo wao dhidi ya Azam FC uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mchezo huo ulipigwa jana jumanne ambapo Azam waliibuka na ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Idriss Mbombo kwa mkwaju wa pelnati.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa alisema kuwa mipango yao waliyoingia nayo kwenye mchezo huo yalitimia kwa asilimia zote.
“Kwanza tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, tumepoteza mchezo lakini pelnati waliyoipata Azam ndio imetuvunja moyo.
“Sina hakika kama ile pelnati waliyoipata ni halali lakini tunaheshimu maamuzi ya mwamuzi.
“Tuliingia na mipango ya kupata pointi tatu au moja kutokana na mpango wetu wa kuzuia ambao ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa.”