Mkwasa Lawama Zote kwa Wachezaji

Kocha Mkuu wa kikosi cha Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amefunguka kuwa matokeo waliyopata jana yametokana na wachezaji kucheza chini ya kiwango.

Jana Ruvu Shooting walipoteza mchezo wa ligi uliopigwa Uwanja wa Uhuru dhidi ya Mbeya City kwa bao 1-0 lililofungwa na Hassan Nassoro.

Akizungumzia mchezo huo, Mkwasa alisema “Kwanza niseme tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, matokeo ya leo yametokana na wachezaji kucheza chini ya kiwango.

“Wachezaji karibu wote kwenye kikosi walicheza chini ya kiwango kitu ambacho kimeigharimu timu kukosa matokeo licha ya nafasi nyingi ambazo tumezitengeneza.

“hata bao ambalo tumeruhusu limetokana na umakini mdogo kwenye safu ya ulinzi lakini tunarudi kwenye Uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kuangalia namna ya kurekebisha hilo.

“Hakuna kocha ambaye anapenda timu yake ifungwe lakini inatokea kutokana na makosa ambayo yanafanyika wakati wa mchezo.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.