BAADA ya kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold, Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting amesema kuwa changamoto ni kukosekana kwa baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye kozi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mkwasa alisema “Tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, tumepoteza pointi tatu lakini tunaenda kufanya marekebisho.

“Tumekuwa na matokeo mabaya leo kutokana na wachezaji wangu kushindwa kukosa umakini kwani tulipata nafasi tukasawazisha bao lakini walinzi wakashindwa kuzuia tukaruhusu bao la pili.

“Tunatakiwa kufanya jitihada kubwa kwetu sisi benchi la ufundi pamoja na wachezaji ukizingatia tuna wachezaji 21 kwenye timu na wengine wapo kozi hivyo wakati mwingine wanakuwa na uchovu nadhani viongozi wanapaswa kulifanyia kazi ili tuwapate waongeze nguvu kwenye kikosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa