Jeremiah Kisubi Mlinda mlango wa Polisi Tanzania ambaye alishawahi kupita Simba SC na kuhudumu kwa msimu mmoja tu, amevunja ukimya kwa kumpa ushauri kipa wa Yanga SC Djigui Diarra.

Kisubi Amshauri Diarra

Baada ya mechi ya mwisho ya Yanga kumaliza kwa sare ya 2-2 kati ya Yanga SC dhidi ya Azam FC, ambapo mlinda mlango huyo wa Yanga SC aliruhusu goli mbili na kufikisha jumla ya goli 4 za kufungwa kwenye mechi 3 alizocheza mpaka sasa.

Kisubi kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika hivi:

“Nilipo kuona katika ligi inayozidi kujiongezea umaarufu, nilivutiwa nawe maana wewe ni golikipa mwenye umbile dogo kama langu Ila kuna vitu wewe ulivijaza zaidi kutetea umbile lako na kuwa Bora zaidi”.

Kisubi Amshauri Diarra

“Na ulipo chukua tuzo ya golikipa Bora msimu uliopita ulistahili kabisa ila nina jambo la kukushauri, kwa sasa apa kwetu uvumilivu hakuna na hawajui vipindi vya mpito kwa mchezaji. Hivyo Kaka nyuma yako kuna shida kubwa ambayo mimi na wewe hatuijui ila shida ipo”.

“Nikuombe kabla Mambo hayajawa mabaya zaidi omba Kwanza hata wiki moja ya kwenda kujitafakari nyumbani, huchezi vibaya ila goli lako limekuwa jepesi na timu yako ina presha kubwa, kama sio ushauri mzuri kwako nisamehe pamoja na timu kwa ujumla msiniwazie mabaya napenda kazi ya huyu mwamba naumia”.

Kisubi Amshauri Diarra

Kisubi ni golikipa wa kitanzania anayefanya vizuri na mwenye kipaji ambacho kiliwavutia Simba SC kumsajili kipindi hicho akiwa Tanzania Prisons, lakini mara baada ya kufika mitaa ya Msimbazi hakuwa na wakati mzuri wa kuonesha kipaji chake na kuomba uongozi wa timu hiyo kumwachia huru akatafute changamoto nyingine, na ndipo aliposajiliwa tena na timu ya Polisi Tanzania ya Moshi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa