Golikipa wa Simba aliyesajiriwa na klabu ya Polisi Tanzania Jeremiah Kisubi ameiomba klabu hiyo iweze kumwachia ili apate nafasi ya kucheza kwenye timu yake hiyo mpya.

Kisubi amejiunga na Polisi kwenye dirisha hili kubwa la usajili akitokea Mtibwa Sugar ambapo alikuwa akiichezea kwa mkopo kwenye msimu ulioisha na kurejea kwenye klabu yake ya Simba.

Simba, Kisubi Aipigia Magoti Simba, Meridianbet

Akizungumzia hilo, Kisubi amesema kuwa “Nimejiunga na Polisi Tanzania ni furaha kwangu kwani nitapambana ili nipate nafasi ya kucheza.

“Bado nina mkataba na Simba ni mkataba mrefu sio wa mwaka mmoja tu ila nimewaomba viongozi waniachie ili nipate nafasi ya kucheza hivyo kama kila kitu kitakuwa sawa basi wao wenyewe wataongea.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa