BAADA ya mechi ya kirafiki dhidi ya Friends Ranger (0-0), Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Joslin Sharif anatarajia kupitisha panga kwa baadhi ya wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho kwa sasa.

Mchezo huo wa kirafiki ulichezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru, ambapo baadhi ya wachezaji kutoka nchini Burundi walikuwepo kwa ajili ya kufanya majaribio.

Chanzo chetu kutoka Polisi kimefunguka kuwa “Kocha atafanya maamuzi ya mwisho kwa wachezaji wanaofanya majaribio leo (jana) baada ya mechi ya kirafiki ili kujua wanaobaki na watakaoondoka.

Akizungumzia hilo Kocha Joslin amesema kuwa “Unajua nilivyofika nilikawia kidogo nikakuta tayari timu ni kama imemaliza kufanya usajili.

“Imenibidi nichukue muda kuangalia wachezaji na viwango walivyonavyo ndio maana unaona tunacheza mechi ya kirafiki ili nione watanisaidia nini kwenye ligi.

“Wale wachezaji ambao wanafanya majaribio kwa sasa wote nawaangalia ili nijue ni wangapi nitakuwa nao ili kuongeza nguvu kwenye kikosi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa