Kambi ya Yanga imezidi kuongezea morale baada ya wachezaji wake waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania kujumiaka na kikosi cha kwanza kwenye viwanja vya Avic Town kigamboni jana Jumanne

Kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi iliingia kambini mapema mwezi Julai kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa ligi kuu lakini ile michuano ya kimataifa.

Yanga, Yanga Mambo Safi Baada ya Kurejea Wachezaji wa Taifa Stars, Meridianbet

Nyota hao waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ni Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Farid Mussa, Feisal Salum, Aboutwalib Mshery, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.

Wachezaji hao wamekamilisha idadi ya nyota ambao watakuwepo ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu ujao huku wakitarajia kucheza mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Polisi Tanzania.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa