USIKU wa kumkia leo Ijumaa palifanyika sherehe za ugawaji tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), msimu wa 2021-22, zilizotolewa katika ukumbi wa Rotana Hotel, Dar es Salaam. Yanga watamba kwenye tuzo hizo.

Tuzo hizo ziligawanyika katika makundi mbalimbali, zikiwemo kikanuni za mashindano, binafsi za wachezaji na waamuzi, kiheshima na kiutawala zikihusisha wasimamizi wa mpira wa miguu na wadau wengine waliotoa mchango wao kwa mchezo huo.

Ambapo kwenye tuzo hizo Yanga walitawala zaidi kwani walitarajiwa kutoa wachezaji wengi ambao wangeondoka washindi.

Kwani wapo wachezaji kama Yanick Bangala walionekana kuwa na nafasi ya kuchukua tuzo zaidi ya moja. Yanga waliondoka na tuzo ya Bingwa wa Kombe la Shirikisho la (ASFC). Kocha wao Nasreedin Nabi alitarajiwa kubeba tuzo ya kocha bora na alionekana kabisa hana mpinzani.

Yanga walikuwepo pia kwenye kuwania tuzo ya timu yeye nidhamu. Kipa Djigui Diara wa Yanga alikuwa kwenye nafasi ya kuwa kipa bora wa msimu baada ya kuwa na rekodi bora dhidi ya kina Aishi Manula.

Beki Bora Ligi Kuu Bara iliwaniawa na Djuma Shaaban akiwa na Henock Inonga wa Simba na Bakari Mwamnyeto wa Yanga wakati tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Bara, Yanick Bangala, Feisal Salum na Salumu Abubakary ‘Sure Boy’ wote wa Yanga.
Ambapo Bangala na Djuma walionekana kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuibukia kidedea.

Yanga wakatokea tena kwenye Tuzo ya Mchezaji Bora wa ASFC, Feisal na Fiston Mayele wakiwa na Abdul Sopu. Wakafanya hivyo tena kwenye Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara.

Yanga Watawala Tuzo za NBC, Bangala, Mayele Wang'aa

Bangala na Mayele waliiwakilisha Yanga tena, huku Bangala akipewa nafasi zaidi dhidi ya Mayele na Inonga wa Simba. Mbali na tuzo ya mchezaji mmoja mmoja.

Yanga walitarajiwa kutoa wachezaji wengi kwenye kikosi bora cha msimu, Diarra, Bangala, Feisal, Dickson Job, Djuma Shaban, Fiston Mayele, Sure Boy na Mwamnyeto ni wachezaji ambo walionekana kustahili kuwepo kikosi.

Kwa ujumla zilitolewa tuzo zaidi ya 57, ikiwemo na wale waliofanya vizuri kwa upande wa Ligi Kuu ya Wanawake Bara. Zilitolewa tuzo za heshima, seti bora ya waamuzi, makamishina wa mechi na watu wenye mchango kwenye soka.

Kipa bora

Diarra Djigui amefanikiwa kutwaa tuzo ya kipa bora wa msimu uliomalizika kwa kuwalaza chali makipa wengine Aish Manula wa Simba na Khomein Abubakar wa Geita Gold.

Beki Bora

Henock Inonga Baka amefanikiwa kutwaa tuzo ya beki bora wa msimu wa NBC mara baada ya kuwapiku wachezaji Djuma Shabani na Bakari Mwamnyeto wa Yanga.

Kiungo Bora

Kwa upande wa kiungo bora wa msimu Yanick Bangala Litombo amefanikiwa kutwaa tuzo ya kiungo bora wa NBC mara baada ya kuwapiku Feisal Salum na Sure Boy wa Yanga.

Kocha bora

Nasreddine Nabi kocha wa Yanga amefanikiwa kutwaa tuzo ya kocha bora wa msimu kwa kuwapiku makocha wengine Juma Mgunda wa Coastal Union na Fred Minziro wa Geita Gold.

Sopu abeba tuzo mbili

Katika hatua nyingine mshambuliaji mpya wa Azam FC ambaye alikuwa akiiwakilisha Coastal Union Abdul Sopu alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Shirikisho na mfungaji bora wa michuano hiyo.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa