Kocha mkuu wa Manchester United Erik ten Hag amefunguka kwamba Harry Maguire ataendelea kuwa nahodha wa timu hiyo kwa msimu ujao alithibitisha hilo wakati wa mkutano na wandishi wa habari huko Bangkok nchini Thailand.
Maguire hakuwa na msimu mzuri chini ya Ole Gunnar Solskjaer na hata kwa Ralf Rangnick akiwa sehemu ya kupoteza kwa Man United kwenye mechi nyingi hali iliyopelekea mashibiki kumtaka mchezaji huyo aondoke na wengine walifikia kumtishia maisha endapo ataendelea kucheza.
Lakini ni kama amekubalika chini ya mwalimu Ten Hag ambapo sasa imetibitika ataendelea kuisimamia timu hiyo ndani ya uwanja na Muholanzi Ten anadhamira ya kuongeza beki wa kati Lisandro Martinez iliashirikiane na Maguire.
Ten Hag alisema: “Nilipaswa kuwajua wachezaji wote lakini yeye tayari amejitambulisha vizuri kama nahodha na amefanikisha mafanikio mengi.
“Labda tumuunge mkono na kuacha kumzomea kocha mpya anampenda.” Alijibu Neville kupitia Twitter.