Antonio Conte kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutulia na kumuunga mkono kwa katika maamuzi anayoyafanya katika klabu hiyo juu ya kikosi chake.

antonio conteMashabiki wa klabu ya Spurs wamekua wakimlaumu mwalimu juu ya uamuzi wake wa kutompa nafasi kijana Djed Spence aliyetoka katika klabu ya Middlesbrough mwezi Julai na kutopata nafasi mara kwa mara huku mbrazil Emerson Royal akiwa anapata nafasi mara kwa mara na mashabiki hao kuamini hatoshi kwenye nafasi na inabidi Spence aanze kupewa dakika za kutosha.

Hii imekuja baada ya Emerson Royal kupata kadi nyekundu katika mchezo wa jumamosi dhidi ya klabu ya Arsenal na kusababisha klabu hiyo kupoteza mchezo huo kwa magoli matatu kwa moja kitu kilichowafanya mashabiki wa klabu hiyo kukasirishwa zaidi na mchezaji huyo licha ya kutokua na muendelezo wa kiwango bora kwenye michezo mingine pia.

Kutokana na hali hiyo kocha Antonio Conte ameamua kufunguka na kueleza zaidi “Mimi sio mjinga, na naweza kufundisha soka kwa watu wengi” Antonio Conte wakati anatetea uamuzi wake kutompa nafasi Djed Spence.

antonio conteBadala ya kutupa lawama kwa mchezaji mmoja aliepata kadi nyekundu Antonio Cote ameendelea kusisitiza zaidi walifanya makosa kama timu kitu kichowagharimu pia kushindwa kutumia nafasi walizopata katika mchezo ndio sababu iliosababisha kupoteza mchezo huo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa