Antonio Conte kocha wa klabu ya Tottenham Hotspurs amesema timu yake haikustahili kupoteza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliopigwa nchini Ureno dhidi ya Sporting CP kwa mabao mawili kwa bila.

Kwenye mchezo huo ambao ilionekana Spurs kuumiliki kwa kiwango kikubwa lakini kitu cha kushangaza walikuja kuruhusu magoli mawili ya usiku kabisa na kujikuta wamepoteza mchezo huo.

antonio conteConte anasema “Kwenye kipindi cha kwanza mchezo ulikua sawa kwa timu zote mbili lakini kwenye kipindi cha pili tulitengeneza nafasi ambazo tungezitumia na kuweza kupata magoli na kushinda mchezo, Lakini kwa bahati mbaya hatukuweza kufanya hivo na kuruhusu kushambuliwa kwa kushtukiza na kipa wangu Lloris kuokoa na mpinzani kupata kona ambayo ilizaa bao”.

Baada ya hapo Spurs waliruhusu goli lingine dakika za nyongeza na kufanya matokeo kua goli mbili kwa bila,Conte aliongeza kwa kusema “Kila siku naongea na wachezaji wangu kitu cha msingi ni matokeo ya mwisho nafikiri labda hatukstahili kupoteza mchezo huu na wakati huohoo hatukustahili kufungwa kwenye mchezo huu”.

“Tunaenda kuangalia tumekosea wapi turekebishe na tumepatia wapi ili tufanyie kazi zaidi michuano ya ulaya ni michuano ya hali ya juu hivo ukifanya makosa yanakugharimu kama yalitugharimu sisi usiku wa leo”.

Tottenham baada ya kupoteza mchezo wa jana usiku dhidi ya Sporting Lisbon wana kazi ya kufanya katika mchezo ujao dhidi ya mabingwa watetezi wa michuano ya Europe league Enchtrackt Frankfurt ili kupata alama sita katika mchezo unaofuata ili kuweza kuweza kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa