STRAIKA mpya wa KMC, Bigirimana Blaise ameanza mazoezi na kikosi hicho baada ya kupona majeraha ya nyama za paja.

Bigirimana

Bigirimana alijiunga na kikosi cha KMC kwenye dirisha kubwa la usajili akitokea Namungo ambapo hakupata nafasi ya kucheza baada ya kuvunjika mguu.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa “Kikosi kinaendelea vizuri na maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ihefu ambao tutacheza Septemba 17.

“Mchezaji wetu ambaye alikuwa akisumbuliwa na majeraha, Bigirimana Blaise ameanza mazoezi na wenzake na kila mchezaji anatamani kwenye mchezo ujao basi tupate pointi tatu.

Bigirimana

“Morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo huo na tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani siku ya jumamosi kwa ajili ya kuisapoti timu yetu ili kuhakikisha tunapata ushindi.”


Kwa habari na matukio ya kimichezo na ya uhakika tembelea Youtube channel yetu Meridian Sport

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa