ALIYEKUWA kipa wa Simba, Jeremiah Kisubi ameongeza mzuka kwenye kikosi cha Polisi Tanzania baada ya kurejea mazoezini baada ya kupona majeraha.

Kisubi alisajiliwa na Polisi Tanzania kwenye dirisha kubwa la usajili akitokea Mtibwa Sugar ambapo alikuwa huko kwa mkopo akitokea Simba.

Kisubi, Kisubi Aongeza Mzuka Polisi, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa “Kikosi kimewasili salama Pwani na tunatarajia kucheza mechi dhidi ya Ruvu Shooting siku ya Ijumaa.

“Katika msimu uliopita tulivuna alama nne, hivyo malengo yetu kuelekea kwenye mchezo huu ni kwenda kuanza ligi kwa kupata ushindi kwao japo tunaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na matokeo waliyoyapata wapinzani wetu kwenye mchezo wao wa mwisho.

“Kocha ameridhika na muunganiko wa vijana wake baada ya michezo mitatu ya ligi na kurejea kwa nyota wake sita kati ya saba waliokuwa majeruhi ambao ni Jeremiah Kisubi, Tariq Simba, Fredy Tangalu, Jamali Mtegeta, James Mwasote na Chilo Mkama.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa